CAPE TOWN-Serikali kupitia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imeingia makubaliano na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake linaloshughulikia masuala ya Madini ya Metali, Gesi na Mafuta (JOGMEC) kufanya tafiti za Miamba na Madini nchini Tanzania.
Makubaliano hayo yamefikiwa kupitia kikao kilichofanyika Februari 6, 2024 jijini Cape Town, Afrika Kusini baina ya taasisi ya GST na Shirika la JOGMEC.
Kwa upande wa Tanzania, imewakilishwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, Kamishna wa Madini, Dkt. AbdulRahman Mwanga, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba na Mkurugenzi wa Kanzidata ya Taarifa za Madini,Bi. Hafsa Maulid.
GST inashiriki Mkutano wa Mining Indaba unaoendelea jijini Capetown, nchini Afrika Kusini ulioanza tarehe 05 Januari na unategemea kufikia tamati tarehe 08 Februari, 2024.
Tags
Habari
Indaba Mining
Investing in African Mining Indaba
JOGMEC of Japan
Kimataifa
Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST)