India yatangaza neema zao la mbaazi Tanzania

NEW DELHI-Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeruhusiwa kuiuzia India kiasi cha mbaazi inachoweza kuanzia sasa hadi Machi, 2025.
Makubaliano hayo yamefikiwa leo tarehe 24 Februari 2024 wakati wa mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba, na Mwenyeji wake Waziri wa Biashara na Viwanda wa nchini humo Mhe. Piyush Goyal yaliyofanyika jijini New Delhi.

Kadhalika, katika mazungumzo hayo viongozi hao wamekubaliana Tume ya Pamoja ya Biashara kukutana mwezi Aprili 2024, ili kuweka mikakati ya pamoja ya kukuza biashara baina ya Tanzania na India.

Awali kabla ya kufikiwa kwa makubaliano haya, Tanzania iliruhusiwa kuuza kiasi cha tani laki mbili pekee kwa mwaka za mbaazi nchini India.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifurahia jambo na Waziri wa Biashara na Viwanda wa India Mhe. Piyush Goyal walipokutana kwa mazungumzo jijini New Delhi.

Waziri Makamba alikuwa nchini India kushiriki Mkutano wa Raisina 2024 sambamba na kufuatilia utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyoifanya nchini humo mwezi Oktoba 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news