ABIDJAN-Dimba la Olympic Stadium of Ebimpé jijini Abidjan, Ivory Coast limewapa heshima wenyeji hao wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2023.
Ni kupitia fainali ya moto ambayo ilipigwa dimbani hapo Februari 11,2024 dhidi ya Nigeria
The Elephants waliwachapa Super Eagles mabao 2-1. Mafanikio ambayo yamewawezesha Ivory Coast kuweka kibindoni dola milioni saba huku Nigeria ikijikusanyia dola milioni nne.
William Troost-Ekong anayechezea PAOK ya Ugiriki alianza kuifungia Nigeria dakika ya 38, kabla ya kiungo wa Al Ahli ya Saudi Arabia, Franck Yannick Kessié kuisawazishia Ivory Coast dakika ya 62.
Straika wa Borussia Dortmund, Sebastien Haller alikuwa shujaa wa Ivory Coast wakati The Elephants walipotoka nyuma na kuwashinda Super Eagles dakika ya 81.