Katibu Mkuu Abeida amjulia hali mtoto aliyekuwa anapigwa na mama yake wa kambo

ZANZIBAR-Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar,Bi. Abeida Rashid Aballah amesema, mtoto Farhia Omar Mohamed (10) ambaye aliyekuwa anapigwa na mama yake wa kambo huko Bububu, Unguja hali yake inaendelea vizuri.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Zanzibar,Abeida Rashid Aballah akiwa na mtoto Farhia Omar Mohamed (10) ambaye aliyekuwa anapigwa na mama yake wa kambo huko Bububu, Unguja na hatimaye mtoto huyo kuchukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzimbar kupitia wizara hiyo

Ameyasema hayo wakati alipomtembea mtoto huyo katika nyumba ya kulea watoto Mazizini, Unguja.

Bi.Abeida amesema, mtoto Farhia atapatiwa haki zake zote za msingi kama sheria ya mtoto inavyoeleza.

Amefahamisha kwamba, Sheria ya Mtoto Na. 2 ya mwaka 2011 imeainisha haki za mtoto ikiwemo haki ya kupata elimu, matibabu, kuishi, nk.

Ameeleza ni wajibu wa Wizara ya Maelendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo kwa maslahi ya taifa.

Katibu Mkuu Abeida ametoa wito kwa wazazi na walezi kutumia busara zaidi wakati wa kumuadhibu mtoto endapo amefanya kosa, kwani ikumbukwe kwamba mtoto ni wa Serikali,hivyo Serikali haitovumilia kuona mtoto anafanyiwa vitendo vya udhalilishaji wa aina yeyote ikiwemo kupigwa, kunyanyaswa, kutelekezwa, n.k.

Mtoto Farhia Omar alichukuliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na kuhifadhiwa katika malezi bora, siku ya Jumapili ya Februari 11,2024

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news