Katibu Tawala Mkoa wa Iringa akabidhiwa vitendea kazi

DODOMA-Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bi. Doris N. Kalasa ameapishwa Februari 2, 2024 na Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dodoma.
Mara baada ya kuapishwa aliwasili Ofisi ya Rais-TAMISEMI ambapo alipokelewa na Mwenyeji wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Bw. Sospeter M. Mtwale na kupatiwa vitendea kazi.

"Umepewa Miundo na Miongozo ya kazi, Ofisi ya TAMISEMI ni Wizara ya Wananchi ipo kila sehemu, ukafanye kazi na wenzako kwa kushirikiana na kimsingi nikuhakikisha mtakuwa mnamsaidia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi, ukajue mila na desturi za sehemu yako ili uweze kuongoza kwa weledi na usichoke kujifunza," alisema Mtwale.

Kwa upande wake, Bi. Kalasa amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua huku akisisitiza kuwa yeye ni muumini wa ushirikiano na anategemea kupata ushirikiano mkubwa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI.

Sambamba na ofisi yake mpya ili aweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu, na kuongeza kuwa hatachoka kujifunza katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news