DODOMA-Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Madini na Taasisi za Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) na Tume ya Madini leo Februari 15, 2023 wamekutana na ugeni wa Kidplomasia kutoka Ubalozi wa Ufaransa nchini na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti ya Ufaransa (BRGM).
Lengo la ugeni huo lilikuwa ni kutambua fursa za uwekezaji hususan kwenye madini muhimu na mkakati na kuangalia maeneo ya ushirikiano katika Sekta ya Madini nchini.


Akizungumza katika kikao hicho, Naibu Katibu Mkuu Mbibo ameueleza ujumbe huo kuwa bado ipo nafasi ya kukutana na kuendeleza ushirikiano baina yao na GST katika maeneo yaliyokubalika.