DAR ES SALAAM-Young Africans Sports Club (Yanga SC) imepigwa faini ya shilingi milioni 2 katika makosa mawili tofauti yanayouhusu michezo miwili ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Februari 15, 2024 na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF)
Kwa mujibu wa taarifa hiyo,kosa la kwanza ambalo faini yake ni shilingi milioni 1 ambalo linatokana na mashabiki wake watatu kuonekana kwenye eneo la vyumba vya kuvalia.
Ni katika mchezo dhidi ya Tanzania Prison ambapo ni kinyume na taaratibu za michezo.
Imeeleza kuwa, adhabu hiyo imezingatia kanuni ya 17:50 na 17:60 ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za mchezo.
Pia, Yanga imetozwa faini nyingine ya shilingi milioni 1 kwa kosa la wachezaji wake kuchelewa kurejea uwanjani katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji FC.
Hali iliyosababisha mchezo kuchelewa kuanza kipindi cha pili kwa dakika saba.