NA SILVIA ERNEST
BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma limeridhia na kupitisha rasimu ya mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/2025 wenye makadirio ya mapato na matumizi ya shilingi 43,884,045,000.
Rasimu hiyo imewasilishwa katika kikao maalum cha baraza kupitia randama ya bajeti ya matumizi ya kawaida na mpango wa maendeleo kwa mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika Februari 1,2024 katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Kigonsera.
Mchanganuo wa makadirio hayo ni ukusanyaji na matumizi ya mapato ya ndani Tshs. 8,400,000,000 ambapo mapato halisi ni Tshs. 6,800,000,000 na mapato fungwa ni Tshs. 1,600,000,000.

Mikakati iliyokwekwa na halmashauri katika ukusanyaji wa mapato kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ni pamoja na kuongezwa kwa idadi ya POS za kukusanyia mapato, kukarabati Soko la Ruanda na jengo la uwekezaji lililopo Mbinga Mjini ili kuchochea biashara zitakazopelekea kuongezeka kwa mapato.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga, Mhe. Deusderius Haule amewataka wataalamu na madaiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kushirikiana na kuimarisha usimamizi katika uukusanya mapato ili kuweza kufikia malengo ya halmashauri.