DODOMA-Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Mwanaisha Ng'anzi Ulenge ameitaka Serikali kuongeza nguvu katika uwekezaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT Hub) ili kuibua ajira kwa vijana.
Wito huo unajiri ikiwa Serikali imepanga Tanzania kuwa kitovu cha maendeleo ICT Hub Afrika Mashariki kwa kuwa mitandao ya kimataifa (Submarine Cables) imeanzia Tanzania na kugawanyika kwa nchi zingine za Afrika.
Ameyasema hayo Februari 5,2024 katika Bunge la 12 mkutano wa 14 kikao cha tano wakati akichangia taarifa ya mwaka bungeni jijini Dodoma.
"Sasa hivi hakuna namna ya kurudi nyuma Dunia imeshatekwa kwa suala la TEHAMA na Teknolojia ya Habari na sisi Tanzania tumeishaingia huko. Nilipongeze Bunge letu tulipitisha Sheria ya Ulinzi Binafsi.
"Lengo la sheria ile ni kuhakikisha mwananchi mmoja mmoja anakwenda kunufaika na uchumi wa kidigitali."
Amesema, Serikali imefaiya jitihada mbalimbali kuhakikisha na sisi tunaingia huko.
"Na hili la sheria ni mojawapo, lakini niiombe sana Serikali na niishauri ihakikishe ili mwananchi mmoja mmoja ananufaika.
"Hatuwezi kwenda kuingia kwenye ulimwengu wa kiteknolojia na kunufaika na uchumi wa kidigitali kama kila mwananchi hataweza kuwa na Digital Identify.
"Serikali imeweka mipango katika Sheria ya Ulinzi Binafsi tuliipitisha lengo lake ni kuhakikisha taarifa za mtu binafsi zilizoko sehemu mbalimbali zinaweza kuwa accessed na kumnufaisha Mtanzania.
"Mfano sasa hivi unaweza kwenda benki ukakopeshwa kulingana na kinachoonekana kilichopo ndani ya benki. Lakini benki inaweza kumkopesha Mtanzania kwa kutumia fedha zake zinazopita kila siku, na hiyo ndio maana halisi ya uchumi wa kidigitali,"amefafanua Mbunge Ulenge.
Vile vile amesema, ili tunufaike zaidi tuhakikishe suala la Digital Identify linakamikika.
"Na pili, zipo nchi nyingi duniani zimenufaika na uchumi wa Kidigitali, tutafute technical assistance ili tuanze kunufaika na uchumi wa kidigitali.
"Nilipongeze Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia kwa initiatives mbalimbali ikiwemo kuanzisha Chuo cha TEHAMA jijini Dodoma."
Mbunge huyo amesema, hivi karibuni walishuhudia serikali imeingia makubaliano na wadau watakaosaidia chuo hicho ili kiende kukamilika.
"Kama kuna mahali ambapo Serikali imefanya vizuri kwa vijana wa kitanzania basi ni chuo hiki cha TEHAMA.
"Hili ni jambo moja kubwa sana, sote tunajua Dunia inakwenda kwenye hiyo Artificial Intelligence.
"Dunia inakwenda kwenye Robotic Technology, kila mmoja wetu hapa haimaanishi sio mtaalamu wa TEHAMA hawezi kwenda kusoma bali unaweza kwenda kusoma upate maarifa na ujuzi.
"Chuo hiki sio kama vyuo vikuu vingine, labda vinavyotoa fani mbalimbali kama ICT, Computer Engineering bali chuo hiki kinakwenda kuziba gape lililokuwepo katika ICT knowledge ndio lengo la chuo hiki.
"Vyuo vingine vilivyopo nchini viangalie na kukipa sapoti sio kama competitive na vyuo vingine vinavyotoa kozi hiyo.
"Mheshimiwa Naibu Spika niipongeze Serikali kwa dhamira yake njema, na tayari Mkoa wetu wa Tanga unakwenda kunufaika na ICT Hubs, Mbeya inakwenda kunufaika, Mwanza inakwenda kunufaika, Arusha inakwenda kunufaika,Zanzibar inakwenda kunufaika, Lindi pia.
"Niipongeze sana Serikali, hapa ndipo tunakwenda kutumia TEHAMA kuhakikisha vijana wetu wanazalisha ajira hapa nchini.
"Tutakubalina kwamba kuna watu milioni nane nchini wanatumia smart phone, lakini mafundi wanaotengeneza simu zetu zinapoharibika ni wapi wanakwenda kujifunza?.
"Hivyo, wanafanya kama kwa kubahatisha, ama kwa kipaji,lakini tukianzisha ICT hubs hapa ndio vijana wanakwenda kujifunza kwa kuzalisha vifaa vya ki-TEHAMA pia ajira za vijana wengi zitazalishwa. Jambo hili la ICT hubs kama ambavyo Kanda hizi nane zinakwenda kutekelezwa.
"Tunaomba sana malengo mliyojiwekea Serikali ya kuhakikisha hizi hubs zinashuka kwenye kila wilaya nchini yatekelezwe na yaonekane ni jambo kubwa kwa vijana wa Kitanzania na tushirikiane kuanzia Wizara ya Mipango liweze kusimama.
"Jambo hili liangaliwe na litumie muda mfupi, vile vile niishauri serikali. Sasa hivi kuna matishio duniani ya ku-attack Critical Infrastructure.
"Miundombinu mbalimbali ya ki-ICT imekuwa attacked kama tulivyoona Benki Kuu ya Lesotho mfumo wao ulikiwa hacked ukawa shida katika suala zima la kifedha.
"Tuliona USA mifumo ya hospitali ilikuwa attacked ni lazima kama Taifa tutafute namna ya kuimarisha mifumo yetu dhidi ya wadukuzi.
"Lazima mambo haya yafanyike leo tusisubiri mpaka tunakuwa attacked ndio tunatafuta namna ya kutoka.
"Tuliona pia nchi ya Sir Lanka mfumo ulikuwa attacked ikawa kero kubwa, hebu fikiri inakwenda Mubimbili wagonjwa wote wamelazwa halafu mifumo iwe attacked maana yake itakuwa kero kubwa na maisha yao yanaweza kupotea.
"Kwa hiyo serikali ione namna ya kusimamia mambo haya na utekelezaji wake unakuwa wa haraka,"amefafanua Mbunge Ulenge.