NA DIRAMAKINI
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo amemkabidhi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa vitabu viwili vinavyoelezea miradi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya nwaka 2020-2025 ndani ya Jimbo hilo.
Prof. Muhongo amemkabidhi Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majliwa leo Februari 16, 2024 Bungeni jijini Dodoma.
Aidha, Mheshimiwa Prof. Muhongo anaendelea kuchapisha vitabu vingine hadi mwaka ujao, 2025.
"Tovuti ya jimbo letu www.musomavijijini.or.tz. inazo taarifa muhimu za maendeleo ya Jimbo la Musoma Vijijini. Vitabu hivyo navyo viko kwenye tovuti hiyo,"imeeleza taarifa ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa akipokea vitabu kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo.
Tags
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Habari
Kassim Majaliwa Kassim
Professor Sospeter Muhongo