NA DIRAMAKINI
MIJI inapopanuka na viwanda huchipua, hewa chafu uongezeka, hivyo kutokana na vyanzo vingi vya uchafuzi wa mazingira huchangia kupumua kuwa vigumu na anga kuwa mbaya zaidi.
Kadiri idadi ya Waafrika inavyoongezeka, ndivyo mrundikano wa taka unavyoongezeka.
Aidha,kutokana na mbinu duni za udhibiti wa taka, plastiki na uchafuzi wa mazingira mbalimbali huingia katika mitaa, mito na vitongoji.
Uchafuzi huu unaathiri vibaya mazingira na afya za binadamu.
Kwa mfano, watu huwa hatarini kwa magonjwa ya kupumua, magonjwa yatokanayo na maji, na masuala mengine ya kiafya.
Ripoti ya hivi karibuni ya Numbeo, jukwaa linalotoa taarifa za wakati sahihi kuhusu gharama za maisha, ubora wa maisha, na mambo ya kijamii na kiuchumi duniani kote, imetoa rekodi kuhusu kiwango cha uchafuzi wa mazingira katika miji ya Afrika mwanzoni mwa 2024.
Kielezo cha uchafuzi na kiwango cha uchafuzi hutumika kutoa maarifa kuhusu viwango vya jumla vya uchafuzi vinavyopatikana katika miji.
Takwimu huzingatia mambo kama vile uchafuzi wa hewa na maji, utupaji wa takataka, usafi, kelele, nafasi za kijani kibichi, na hatua kuhusiana na uchafuzi wa mazingira.
Below are the 10 most polluted cities in Africa:
Rank | Country | Pollution index | Exp pollution index |
---|---|---|---|
1 | Cairo, Egypt | 90.9 | 164.0 |
2 | Lagos, Nigeria | 89.0 | 159.0 |
3 | Marrakech, Morocco | 83.5 | 149.3 |
4 | Casablanca, Morocco | 82.2 | 146.6 |
5 | Nairobi, Kenya | 79.8 | 142.3 |
6 | Addis Ababa, Ethiopia | 76.1 | 133.6 |
7 | Alexandria, Egypt | 74.3 | 130.6 |
8 | Tunis, Tunisia | 72.5 | 127.0 |
9 | Johannesburg, South Africa | 61.1 | 106.3 |
10 | Pretoria, South Africa | 55.1 | 94.8 |