ARUSHA-Msajili Hazina, Nehemiah Kyando Mchechu jana Februari 20, 2024 alitembelea Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) iliyopo jijini Arusha, Tanzania.
Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kukagua utekelezaji wa majukumu ya mamlaka hiyo.
TPHPA ilianzishwa kwa Sheria Na. 04 ya 2020 ni miongoni mwa taasisi za umma zilizopo chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina nchini.
Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) imeanzishwa kupitia Sheria ya Msajili wa Hazina (mamlaka na majukumu) sura 370 lengo kuu la kuanzishwa kwa TR ni kusimamia uwekezaji na mali zingine za Serikali katika taasisi na mashirika ya umma.
Sambamba na kampuni ambazo Serikali ina umiliki wa hisa au kuna maslahi ya umma kwa niaba ya Rais na kwa ajili ya Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.