Msajili wa Hazina Zanzibar awashika mkono waathirika wa maafa Hanang'

DODOMA-Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. Jenista Mhagama amepokea mchango wa Msajili wa Hazina kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wa shiliingi milioni 54.3 kwa ajili ya waathirika ya naafa ya maporomoko ya tope, miti na mawe yaliyotokea Disemba 3, 2023 mkoani Manyara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 54.3 kutoka kwa Msajili wa Hazina wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Waheed Mohammad Ibrahim Sanya, kwa ajili ya waathirika wa maafa ya Hanang’, ofisini kwake bungeni Dodoma leo Februari 9, 2024.

Akizungumza baada ya kupokea mfano wa hundi hiyo Ofisini kwake Bungeni jijini Dodoma leo Februari 9, 2024 Waziri Mhagama ameishukuru Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kuguswa kwa kiasi kikubwa na maafa yaliyotokea Hanang’ ambayo yamesababisha watu kupoteza maisha na mali zao na kuongeza kusema kuwa, baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa kutangaza hali ya hatari kabla ya kutokea kwa maafa hayo, Kamati za Maafa za Mikoa zilikuwa zimeshajipanga kwa kutoa elimu na tahadhari.

Aliendelea kusema kuwa, kwa sasa Serikali inatekeleza ahadi yake ya kuwajengea nyumba waathirika wa maafa hayo na maandalizi ya awali yameshaanza kutekelezwa.

Aidha, Waziri Mhagama ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari kwa msimu huu wa mvua za el nino zinazoendelea na kuongeza kusema kuwa msimu wa mvua za masika unakuja hivyo kila mmoja aendelee kuchukua tahadhari.

“Mmefanya jambo kubwa kuungana nasi kwa kuwashika mkono waathirika wa maafa ya Hanang’ kipekee ninawashukuru sana kwa moyo huu na mmeonesha faida za Muungano wetu na mashirikiano tuliyonayo katika hali zote, iwe furaha au majonzi kama haya, ninaahidi kuendelea kutoa ushirikiano nanyi,” alisisitiza Mhe.Mgahama.

Kwa upande wake Msajili wa Hazina wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Waheed Mohammad Ibrahim Sanya alisema, Ofisi yake iliguswa na maafa yaliyotokea Hanang’ na kuona kuna kila sababu ya kuungana kwa kuwashika mkono waathirika hao kwa kutoa mkono wa pole.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news