Mzee Ali Hassan Mwinyi apelekwa hospitali

DAR ES SALAAM-Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Familia,Abdullah Ali Mwinyi ambayo imeeleza kuwa, Mzee Mwinyi anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari.

"Kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu. Hivyo Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala, na Maombi."

Mzee Mwinyi amewahi kuhudumu madarakani kama Rais wa Awamu ya Pili toka mwaka 1985 hadi mwaka 1995, akichukua nafasi ya uongozi kutoka Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kumkabidhi kijiti cha uongozi Hayati Benjamin Mkapa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news