NA GODFREY NNKO
NABII Mkuu, Mheshimiwa Dkt.Geordavie wa Ngurumo ya Upako amewataka Wakristo na Watanzania kwa ujumla kufanya kazi kwa bidii kwani, Mungu huwa anabariki kazi ya mikono ya mtu na si kazi ya maombi yake.
Nabii Mkuu Mheshimiwa Dkt.GeoDavie wa Ngurumo ya Upako jijini Arusha.Wito huo ameutoa hivi karibuni katika moja wapo ya ibada iliyofanyika ndani ya Ngurumo ya Upako (Chuo Kikuu cha Manabii) iliyopo Kisongo jijini Arusha.
"Neno la mtumishi wako kanisani likusaidie wewe kukufanyia wepesi katika kazi za mikono yako ili uweze kupenya kwa haraka, na kufanikiwa kwa haraka.
"Huo ndiyo tunauita muujiza, lakini kutegemea neno la Nabii unasema, Nabii ameshatamka imeshakuwa, mimi ninaenda kulala ninajua Mungu atarekebisha mambo. Unamtuma Mungu akakufanyie kazi? Mungu anabariki kazi ya mikono yako.
"Yaani wewe umuombe Mungu akupe hela, yeye Mungu ndiye anaenda kufanya kazi akupe hela?. Unampa Mungu kazi, akafanye kazi akuletee wewe hela? Ee…Yaani wewe umekaa nyumbani unataka Mungu akafanye kazi akuletee hela, anafanyaje kazi?.
“Unatakiwa kufanya kazi wewe mwenyewe kwa mikono yako, na Mungu anabariki kazi ya mikono yako siyo kazi ya maombi yako.
“Mungu habariki kazi ya maombi yako, anabariki kazi ya mikono yako, yaani miujiza Mungu akupe wewe, wewe umekaa tu bwetee…kila kitu miujiza, aha… kuna vitu vingine ni kwa kufanya kazi,"alifafanua Nabii Mkuu,Mheshimiwa Dkt.Geordavie.
Tags
Acha Injili Iende Mbele
GeorDavie
GeorDavie Ministries Int'l
Habari
Nabii Mkuu Dr GeorDavie
Nabii Mkuu Mhe Dkt.GeorDavie