NA MUNIR SHEMWETA
WANMM
NAIBU Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda ametaka kuwepo upendo miongoni mwa watumishi ili waweze kutekeleza majukumu kwa ufanisi.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza na watumishi wa Ardhi Makao Makuu ya Wizara tarehe 9 Februari 2024 jijini Dodoma.
Aidha, amewataka watumishi hao wa sekta ya ardhi kufanya kazi kwa bidii ili serikali ione matunda na ufanisi wa kazi walizotumwa kuzitekeleza
Mhe Pinda amesema hayo tarehe 9 Februari 2024 jijini Dodoma wakati alizingumza na viongozi na watumishi wa Wizara ya Ardhi Makao makuu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Lucy Kabyemera akizungumza kwenye kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda na watumishi wa wizara ya Ardhi Makao Makuu tarehe 9 Februari 2024 jijini Dodoma.
Amesema, akiwa kama Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi asingependa watumishi wa sekta hiyo kuishi bila upendo ndiyo maana ameamua kukutana na kada zote za sekta ya ardhi kwa lengo la kujua changamoto za watumishi wa kada hizo.
Ameongeza kwa kusema, upendo miomgoni mwa watumishi siyo tu unatoa faraja kwa watumishi bali unarahisisha kazi za wizara kwa kuwa watumishi hao watakuwa wakifanya kazi kwa furaha na amani.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Sheushi Mbuli akizungumza katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda na watumishi wa wizara ya Ardhi Makao Makuu tarehe 9 Februari 2024 jijini Dodoma.
Aidha, amebainisha kuwa, uamuzi wa kukutana na watumishi unalenga pia kuwafunda na kuwaweka karibu watumishi ili wizara ya ardhi ifanye kazi kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya.
"Nimeona nikae na watumishi kwa hekima na busara ili nifahamu changamoto zinazowakabili na kuzitatua ili mwisho wa siku kuondoa malalamiko yanayotolewa kwa wizara.Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Ardhi Makao Makuu wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda tarehe 9 Februari 2024 jijini Dodoma.
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Ardhi Makao Makuu wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda tarehe 9 Februari 2024 jijini Dodoma.
"Shati letu limejaa madoa, ukipita mtaani wakiona mtumishi wa ardhi wanasema ni wale wale na sauti za kulaumu ni kali kweli kweli," alisema Mhe. Pinda.
Vile vile, mhe Pinda ametaka watumishi wa sekta hiyo kupewa stahiki zao kwa mujibu wa sheŕia, taratibu na miongozo iliyopo ili wafanye kazi kwa bidii bila manung'uniko.
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Ardhi Makao Makuu wakiwa katika kikao na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda tarehe 9 Februari 2024 jijini Dodoma. (Picha na WANMM).
"Watumishi wakipewa posho stahiki utaona jinsi wanavyokimbiza mambo na ugumu utaisha," alisema Mhe Pinda.