Nje Jogging mguu sawa Kili Marathon 2024

KILIMANJARO-Ikiwa imebakia siku moja kufanyika kwa mbio za Kimataifa za Kilimanjaro (Kilimanjaro International Marathon 2024) timu ya riadha ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Jogging) imeendelea na maandalizi ya kushiriki mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Februari 25,2024 Moshi, Kilimanjaro.
Wanariadha hao wameweka kambi ya siku tatu mjini Moshi wakijifua na hatua za maandalizi ya mbio hizo.

Kadhalika, Makatibu Wakuu wa Wizara wanatarajiwa kuungana na timu hiyo katika mbio hizo kesho.

Viongozi hao ni Katibu Mkuu, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Said Shaibu Mussa.
Mbio za Kilimanjaro International Marathon 2024 zitafanyika katika Chuo cha Usharika Moshi (MoCU) ambapo zimeandaliwa na Kampuni ya Kilimanjaro Marathon na kuratibiwa kitaifa na Kampuni ya Executive Solutions.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news