Polisi wafunguka madai ajali inayohusishwa na msafara wa Makamu wa Rais

DAR ES SALAAM-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni,SACP Mtatiro N. Kitinkwi amewataka wananchi kupuuza taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii zikidai msafara wa Makamu wa Rais umesababisha ajali leo.
"Mnamo tarehe 21/02/2024 majira ya saa 06:30 huko maeneo ya Tegeta kwa Ndevu barabara ya Bagamoyo gari lenye namba za usajili T.446 DDM na traller T. 527 DDM aina ya Scania likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa majina Saimon Wilfred Laizer (45) mkazi wa Tabora akitokea Mbuyuni kuelekea Tegeta,

"Gari hilo liliacha njia na kugonga kingo za daraja, kupinduka kisha kutumbukia mtoni na kusababisha kifo kwa dereva, uharibifu wa gari na miundombinu ya barabara, chanzo cha ajali kinachunguzwa.

"Zipo taarifa kwenye mitandao ya kijamii kwamba ajali hiyo inahusishwa na msafara wa Mh. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Ukweli ni kwamba ajali hiyo imetokea tarehe 21/02/2024 majira ya saa 06:30 asubuhi wakati msafara wa Mheshimiwa Makamu wa Rais umepita majira ya saa 07:45 asubuhi, takribani saa moja 1 na dakika 15 baada ya ajali kutokea.

"Hivyo taarifa hizo zipuuzwe kwa kuwa hazina ukweli wowote na pia hakuna uhusiano kati ya msafara wa Mheshimiwa Makamu wa Rais na ajali hiyo,"ameeleza SACP Mtatiro N. Kitinkwi.

Aidha,Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni limetoa wito kwa madereva kuzingatia na kufuata kanuni na sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali.

Pia,Jeshi la Polisi limetoa onyo kali kwa wale ambao wanatoa taarifa za upotoshaji zisizo thibitishwa na mamlaka husika ili kuepusha taharuki kwa jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news