NA GODFREY NNKO
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Shariff Ali Sharif kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 13, 2024 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.
“Kwa mujibu wa uwezo waliopewa chini ya kifungu namba 66 cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Mheshimiwa Sharrif Ali Sharif kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi,”imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.
Aidha, kupitia taarifa hiyo, imefafanua kuwa, uteuzi huo wa Mheshimiwa Sharif unaanza leo Februari 13,2024.