ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua Mheshimiwa Sharrif Ali Sharrif kuwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Kazi,Uchumi na Uwekezaji.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena A.Said ambapo uteuzi huo umeanza leo Februari 21,2024.