Rais Dkt.Mwinyi atoa wito matibabu ya saratani

DAR ES SALAAM-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa wadau mbalimbali kutambua umuhimu wa ushirikiano ili kufikia malengo kwa kuwekeza rasilimali fedha katika kuimarisha utafiti, kuboresha miundombinu ya afya, na kuhakikisha upatikanaji matibabu sawa kwa wagonjwa wa saratani nchini.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo Februari 6,2024 katika jukwaa la uwekezaji linalolenga kuimarisha huduma za saratani nchini, ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa, kupitia ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi, watafiti na wataalamu wa tiba kunaweza kubadilisha taswira za huduma za matibabu ya saratani nchini.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali imeanza kuchukua hatua kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo saratani kwa kujenga miundombinu ya huduma za afya, mikakati ya upatikanaji wa huduma bora za matibabu bora kwa wote.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameishukuru Serikali ya Marekani kwa ushirikiano wao kufanikisha utekelezaji wa mipango ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya nchini.

Pia amewashukuru wadau wa Global Health Catalyst ambao wamejitolea kushirikiana na Serikali katika mapambano ya maradhi ya saratani, wawekezaji wa ndani wakiongozwa na Taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF) pamoja na CEO Roundtable kwa utayari walionyesha kushirikiana na Serikali.

Rais Dkt.Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uongozi na jitihada zake za kuimarisha ustawi wa maendeleo nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news