ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi atafanya ziara ya masoko na maeneo ya biashara Zanzibar.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Rais atatembelea soko la mnada wa vyakula Jumbi, soko la samaki Malindi, Bandari ya Malindi na soko la Darajani.
Aidha,katika ziara hiyo Februari 26,2024 atakutana na wafanyabiashara, wachuuzi na wadau mbalimbali wa sekta hiyo.