DODOMA-"Nilipowajulia hali watoto Kareem, Laurean, Deus, pamoja na wagonjwa wengine katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kati ya Benjamin Mkapa, Dodoma. Chini kulia, nikipiga soga kidogo na Ester, ambaye alimchangia uloto mdogo wake anayetibiwa hospitalini hapo.
"Tunaendelea kupiga hatua kubwa katika maboresho ya sekta ya afya nchini ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa hospitali za rufaa za kanda. Huku kazi hii njema ikiendelea, ninayo furaha kuona kuanza kwa utekelezaji wa hatua nyingine muhimu katika eneo hili, ya kusambaza wahudumu wa afya ngazi ya jamii wapatao 137,294 ili kutoa elimu ya afya hadi ngazi ya kitongoji,"amefafanua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan tarehe 1 Februari, 2024.