Rais mpya Namibia atoa kauli ya kushangaza wengi

NA DIRAMAKINI

MAKAMU wa Rais wa Namibia, Nangolo Mbumba, ambaye amechukua wadhifa wa rais wa muda wa nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika siku ya Jumapili baada ya Hage Geingob kufariki akiwa madarakani, amesema hana mpango wa kugombea katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Mheshimiwa Nangolo Mbumba akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu, Peter Shivute (hayupo pichani) Februari 4,2024 Ikulu jijini Windhoek.(Picha na Ikulu).

Kauli hiyo ina maana kwamba Netumbo Nandi-Ndaitwah, ambaye anachukua nafasi ya Mbumba kama Makamu wa Rais na kupendekezwa na Chama tawala cha Umoja wa Watu wa Afrika Kusini Magharibi (SWAPO) zaidi ya mwaka mmoja uliopita kuwa mgombea wake, atasalia kwenye kinyang'anyiro.

Iwapo Netumbo Nandi-Ndaitwah atashinda, atakuwa rais wa kwanza mwanamke katika taifa hilo la Kusini mwa Afrika.

"Sitakuwepo kwa ajili ya uchaguzi,kwa hiyo msiwe na hofu," Mbumba alisema katika hatua ambayo ni nadra miongoni mwa viongozi wa Afrika ambao mara nyingi wamekuwa wakitafuta kila namna kujilimbikizia madaraka mara yanapokuwa mikononi mwao.

"Lengo langu lilikuwa kuwa mkuu wa shule, jambo ambalo nililifanikisha na sasa sina budi kuwashukuru watu wa Namibia kwa heshima waliyonipa ya kuwa rais wao, kwa kipindi kifupi," Mbumba alisema katika hafla ya kuapishwa kwake.

Katiba ya SWAPO inakataza kufanya mabadiliko mara mgombea anapochaguliwa miaka miwili kabla ya uchaguzi kukamilika. 

Chama hicho kimeitawala Namibia, Taifa lenye almasi nyingi, uranium na pia lithiamu inayohitajika kwa betri za magari ya umeme - tangu uhuru kutoka Afrika Kusini mwaka 1990.

Geingob, aliyekuwa madarakani tangu 2015, alifariki akiwa na umri wa miaka 82 mapema Jumapili baada ya kuugua saratani.

"Inatia uchungu na kutia moyo kuona kwamba leo hii, hata katika wakati huu wa hasara kubwa, taifa letu bado limetulia na ni tulivu," alisema Mbumba.

"Hii ni kutokana na uongozi wenye maono ... wa Rais Geingob ambaye alikuwa mbunifu mkuu wa katiba ya Namibia." Geingob anaiacha Namibia nchi ya kipato cha kati inayopigania kusukuma ukuaji wa uchumi zaidi ya asilimia tatu kufuatia kushuka kiuchumi kulikochochewa na janga la UVIKO-19.

Sambamba na kubadilisha ubaguzi wa rangi ulioachwa kutoka kwa ukoloni na kushikiliwa na serikali ya zamani ya wazungu wachache ya Afrika Kusini.

Pia, aliongoza juhudi za Namibia kusonga mbele kama kiongozi wa uchumi wa kijani kibichi na mwaka 2022 Namibia ikawa nchi ya kwanza ya Afrika kukubali kusambaza Umoja wa Ulaya hidrojeni na madini yanayohitajika kwa nishati safi.

Mwaka jana, Namibia ilianza kujenga kiwanda cha kwanza cha chuma, kitakachowezeshwa na hidrojeni ya kijani kibichi pekee ambayo hutolewa kutoka katika maji kwa kutumia mfumo wa electrolysis inayoendeshwa na nishati mbadala.

Maendeleo haya yanaiweka Namibia mbele kiuchumi dhidi ya jirani yake Afrika Kusini mwenye viwanda vingi, ambayo juhudi zake za mabadiliko ya nishati ya kijani zimekuwa zikidorora.

Mheshimiwa Nangolo Mbumba ambaye alizaliwa Agosti 15,1941 huko Olukonda nchini Namibia kwa sasa ana umri wa miaka 82 na anatarajiwa kuliongoza Taifa hilo kwa miezi 10 kabla ya uchaguzi kufanyika. (Reuters/NA)

Taifa hilo tangu Uhuru limeongozwa na marais hawa;

No.Name (Birth–Death)Term of office
Left office
1Sam Nujoma (born 1929)21 March 2005
2Hifikepunye Pohamba (born 1935)21 March 2015
3Hage Geingob (1941–2024)4 February 2024 (died in office.)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news