DAR ES SALAAM-Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mheshimiwa Albert Chalamila ameshiriki hafla ya miaka 50 ya Brahma Kumaris ya kutoa huduma katika Afrika ikiwemo Tanzania.
Ni katika hafla ambayo imefanyika katika Ukumbi wa mikutano wa JNICC jijini Dar es Salaam na kuudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo watu wa jamii ya Kihindi.
RC Chalamila alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye alishindwa kufika kutokana na mwingiliano wa ratiba za kitaifa.
Akiwa katika hafla hiyo RC Chalamila alishiriki matukio mbalimbali kama tukio la kuwasha mshumaa ikiwa ni kumbukizi ya miaka 50 ya Brahma Kumaris toka kuanza kutoa huduma katika nchi za Afrika.
RC Chalamila akiongea na hadhira hiyo amepongeza maandalizi ya hafla hiyo, lakini pia kuchagua hafla hiyo ifanyike hapa nchini hususani Mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema, anajisikia furaha na fahari kujumuika nao katika siku hiyo muhimu na wakati wowote wakiwa na tukio wasisite kumkaribisha.
Vile vile akitoa salamu za Mhe. Rais Dkt.Samia RC Chalamila amesema Rais anawasalimu sana na yuko pamoja.
Pia,angependa kuwa pamoja nao karika tukio hilo, lakini kwa sababu zisizozuilika ameshindwa kuja hivyo anatambua mchango na faida ya uwepo wao hapa nchini kwa masilahi mapana ya Umma ameahidi kuendeleza na kudumisha ushirikiano uliopo.
Mwisho hafla hiyo yenye kauli mbiu " Love, Peace, Unity-Key to Success" ilihudhuriwa na watu mashuhuri akiwemo Balozi wa India, na Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Mhe. Edward Mpogolo.