TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ni Taasisi ya Umma iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya Mwaka 2007.
Sheria hii ilitungwa baada ya kufutwa kwa Sheria ya Kuzuia Rushwa (TAKURU) Sura ya 329 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.
Kuanzishwa kwa chombo hiki kulikuja baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha Mswada wa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa mwaka 2007 mnamo tarehe 16 Aprili, 2007.
Mswada huu ulisainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete kuwa Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mnamo tarehe 11 Juni, 2007 na ilianza kufanya kazi tarehe 1 Julai, 2007.