OSLO-Tanzania na Norway zimetia saini hati ya makubaliano (Memorandum of Understanding- MOU) ya Ushirikiano wa Kilimo na Usalama wa Chakula tarehe 14 Februari, 2024 katika ukumbi wa Climate House (Garden Avenue) Oslo nchini Norway.
Hafla ya kusaini MOU hiyo ilihusisha utiaji saini wa Waziri wa Kilimo,Mhe. Husein Mohamed Bashe (Mb) kwa upande wa Tanzania na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway, Mhe Anne Beathe Tvinnerein ambapo Mhe. Dkt. Samiam Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshuudia hafla hiyo.
Makubaliano hayo yamelenga kuimarisha masuala ya utafiti, biashara ya mazao ya kilimo, kuimarisha vyama vya ushirika na kilimo himilivu kwa mabadiliko ya tabianchi.