TAWA yaunga mkono jitihada za Rais Dkt.Samia wilayani Serengeti, yagusa maisha ya wananchi

NA BEATUS MAGANJA

MKUU wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Dkt. Vincent Mashinji amesema, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imeendelea kuunga mkono jitihada za Baba wa Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha elimu inakuwa kipaumbele wilayani Serengeti.
Dkt. Mashinji ameyasema hayo Februari 01, 2024 wakati wa ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na TAWA kwa kushirikiana na nguvu za wananchi kwa fedha zinazotokana na shughuli za uwindaji wa kitalii, ziara iliyofanywa na TAWA wilayani humo.

"Kwa kumuunga mkono Mhe. Rais TAWA wameweza kutujengea miradi 6 ambayo imejielekeza katika Sekta ya elimu," amesema Dkt. Mashinji.
Akibainisha miradi hiyo Mkuu huyo wa wilaya amesema katika Kata ya Sedeco, vijiji vya Bonchugu na Mbilikiri TAWA wamejenga chumba kimoja (1) cha darasa huku Kata ya Kyambahi Kijiji cha Bokore wamejenga vyumba viwili (2) vya madarasa.

Pia katika Kata ya Manchira Kijiji cha Kazi TAWA wamejenga nyumba moja (1) ya Mwalimu na matundu kumi (10) ya vyoo katika shule ya Msingi Rwamchanga kikiwemo choo kwa ajili ya watu wenye changamoto ya viungo vya mwili (walemavu) pamoja na chumba maalumu cha wanafunzi wakike kwa ajili ya kubadilishia taulo.

Kwa niaba ya wananchi, Diwani wa Kata ya Kyambahi Mhe. Herman Kinyalire amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia TAWA kwa kuwezesha ukamilishwaji wa miradi mikubwa minne (4) katika Kata yake ambayo ni madarasa manne (4), vyumba viwili (2) vya madarasa pamoja na samani za shule.
Aidha, amesema utekelezaji wa miradi hiyo umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza ujangili katika Kata yake na kuwafanya wananchi waongeze ushirikiano katika uhifadhi wa wanyamapori kwa kuwa wanaziona faida za moja kwa moja zinazotokana na shughuli za uhifadhi.
Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA, Beatus Maganja amesema, TAWA haiwezi kuongelea mafanikio wanayoyapata ikiwa ni pamoja utekelezaji wa miradi hiyo bila kuhusisha Jitahada za dhati zilizofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news