TMA yatoa angalizo madhara ya wanyamapori kwa binadamu Masika hii

DAR ES SALAAM-Hali ya malisho na maji kwa ajili ya wanyamapori katika mbuga na hifadhi inatarajiwa kuwa nzuri.
Hayo yamebainishwa leo Februari 22, 2024 jijini Dar es Salaam na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TM) kupitia taarifa ya utabiri wa Masika 2024.

Hata hivyo, mvua za wastani hadi juu ya wastani zinazotarajiwa katika maeneo mengi zinaweza kusababisha kutuama na kusambaa kwa maji na kupelekea kuhama kwa wanyamapori.

"Hali hii inaweza kupelekea magonjwa ya wanyamapori kusambaa kwa wanyama wanaofugwa na binadamu kutokana na wanyamapori kuingia katika makazi ya jamii zinazozunguka hifadhi na mbuga."

Pia, kwa mujibu wa TMA hali hii inaweza kusababisha hatari kwa binadamu na wanyama wanaofugwa kutokana na kushambuliwa na wanyamapori.

"Mamlaka husika zinashauriwa kuboresha miundombinu mbalimbali katika hifadhi za wanyamapori na kujenga uelewa kwa jamii ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.

"Hivyo basi, jamii inashauriwa kutoa taarifa kwa mamlaka husika endapo wanyamapori wataingia katika makazi ya watu."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news