TMA:Wafugaji na wavuvi kunufaika Masika hii,ila...

DAR ES SALAAM-Wafugaji na wavuvi wanatarajiwa kunufaika na upatikanaji wa malisho na chakula cha samaki.
Hayo yamebainishwa leo Februari 22, 2024 jijini Dar es Salaam na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TM) kupitia taarifa ya utabiri wa Masika 2024.

"Hata hivyo, mlipuko wa magonjwa ya mifugo kama vile ugonjwa wa homa ya bonde la ufa na kuzaliana kwa wadudu wanaosambaza magojwa vinaweza kujitokeza."

Vilevile,kwa mujibu wa TMA matukio ya kuongezeka kwa magonjwa ya mwani baharini na kupungua kwa uzalishaji wa mwani kutokana na kupungua kwa kiwango cha chumvi ya maji ya bahari vinatarajiwa.

Aidha,wafugaji wanashauriwa kutumia mbinu bora za ufugaji ili kutunza malisho na kuvuna maji ya mvua kwa matumizi ya baadae.

"Jamii inashauriwa kuweka mipango mizuri ya matumizi bora ya maji na malisho.

"Wakulima wa mwani wanashauriwa kulima mwani kwenye maji ya kina kirefu ili kuondokana na athari za maji ya mvua yanayokuwa yanaingia baharini.

"Vilevile, wafugaji na wavuvi wanashauriwa kufuatilia mirejeo ya tabiri za hali ya hewa na ushauri kutoka kwa maafisa ugani ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza na kuongeza tija katika msimu huu wa mvua,"imeeleza taarifa hiyo ya TMA.

Kwa mujibu wa TMA,kwa ujumla mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

Aidha,ongezeko la mvua linatarajiwa mwezi Machi, 2024 katika maeneo hayo.

"Kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, na Mara) pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma (wilaya za Kakonko na Kibondo).

"Mvua za masika zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Kigoma."

Vile vile,mvua za nje ya msimu zinazoendelea kunyesha zinatarajiwa kuungana na mvua za Masika 2024.

TMA imebainisha kuwa,mvua zinatarajiwa kuisha wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei, 2024.

Wakati huo huo, kwa upande wa Ukanda wa Pwani ya Kaskazini (Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Mkoa wa Pwani (ikijumuisha kisiwa cha Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, TMA imebainisha kuwa,mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini.

"Mvua hizo zinatarajiwa kuanza mapema wiki ya nne ya mwezi Februari, 2024 na kuisha wiki ya tatu na ya nne ya mwezi Mei, 2024."

Kwa upande waNyanda za Juu Kaskazini Mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro), mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani na zinatarajiwa kuanza mapema wiki ya nne ya mwezi Februari, 2024.

"Mvua hizo zinatarajiwa kuisha wiki ya pili na ya tatu ya mwezi Mei, 2024,"imeeleza taarifa hiyo ya TMA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news