TRRH yapokea vifaa tiba maalumu

DAR ES SALAAM-Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke (TRRH) imepokea vifaa tiba maalumu kutoka Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Global Fund kwa ajili ya kuhudumia watoto waliozaliwa kabla ya muhula.

Vifaa hivyo, vyenye thamani ya shilingi milioni 52, vinawezesha matibabu ya watoto waliozaliwa chini ya wiki 32 wanaokabiliwa na matatizo kama upuaji, homa ya mapafu, maambukizi kwa watoto wachanga wenye shida ya kupumua, na kujaa kwa maji katika mapafu.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dkt. Joseph Kimaro, ameshukuru kwa msaada huo wa vifaa tiba kutoka Global Fund na ameeleza umuhimu wa vifaa hivyo katika kutoa huduma bora za matibabu kwa watoto waliozaliwa kabla ya wakati.

Amesisitiza kuwa, vifaa hivyo vitasaidia katika kushughulikia changamoto mbalimbali za kiafya ambazo watoto hawa wanaweza kukumbana nazo, na hivyo kuongeza nafasi zao za kupona na kuishi maisha yenye afya njema.

Dkt. Kimaro ametoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huu na kuchangia katika kuboresha huduma za afya kwa jamii, hususan kwa makundi yanayohitaji msaada zaidi kama watoto wachanga

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke(TRRH) ina wodi maaluumu ya kuhudumia watoto wachanga na hasa wale waliozaliwa kabla ya muhula hivyo kupitia ongezeko la vifaa hivyo hakika utoaji huduma kwa watoto wachanga unazidi kuimarika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news