Ukiwajibika,lazima uwe mkweli-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka viongozi mbalimbali kuongeza kasi mara mbili kuwatumikia wananchi pamoja na kukamilisha ahadi na kuvuka utekelezaji.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo Februari 1,2024 katika hafla fupi ya kuwaapisha Mawaziri na Manaibu Waziri wapya aliowateua hivi karibuni viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amemtaka Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale, Mhe.Mudrick Ramadhan Soraga kuweka juhudi kubwa kupanua wigo katika Sekta ya Utalii hususan utalii wa urithi, mikutano na michezo.

Vilevile, Rais Dkt. Mwinyi amemtaka Waziri mpya wa Wizara ya Uchumi wa Buluu, Mhe. Shaaban Ali Othman kuongeza juhudi katika kuzitatua changamoto za wananchi na kukuza vipato vyao pamoja na fursa za mafuta na gesi katika sekta hiyo.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amewaagiza Wizara ya ardhi kutatua migogoro ya ardhi.

Rais Dkt.Mwinyi amesema, kujiuzulu kwa Waziri si jambo geni ni njia ya uwajibikaji, ameeleza kuwa, wakati mtu anawajibika kujiuzulu lazima kuwa mkweli kama kuna sababu za mgongano wa kimaslahi atangaze na kusema wazi sababu zilizomfanya awajibike.

"Sababu nyingine ya waziri kujiuzulu ni pale ambapo serikali inaamua jambo na wewe ukubaliani nalo, unatoka unajiuzulu kwa sababu ukubaliani na maamuzi yaliyotolewa na serikali.

"Lakini kuna jambo moja lazima tukumbushane wakati unawajibika kwa njia yeyote ile ya kwanza au ya pili ni lazima uwe mkweli na ukweli naozungumzia hapa ni kama kuna mgongano wa maslahi utangaze.

"Kama tumezuia kitu na wewe una biashara hiyo tangaza, sema ukweli, sema ukweli hapa kuna mgongano wa kimaslahi mimi ni muagizaji wa kitu fulani na ninyi mmezuia, lazima tuwe wa kweli sasa hivi ukitoka halafu ukaenda kuwaamisha watu kinyume chake si sahihi,”amesisitiza Rais Mwinyi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news