Ushirikina watajwa kuwakimbiza walimu nyumba za Serikali

NA FRESHA KINASA

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara, Msongela Palela amesema kuwa, moja ya sababu inayochangia baadhi ya walimu katika halmashauri hiyo kuogopa na kushindwa kukaa kwenye nyumba ambazo zimejengwa na Serikali katika vituo vyao vya kazi ni imani za kishirikina.
Ameyasema hayo Februari 16, 2024 wakati akijibu hoja hiyo,kufuatia baadhi ya madiwani kutaka kujua kwa nini baadhi ya walimu wamehama katika baadhi ya nyumba ambazo serikali imezijenga katika vituo vya kazi kwa ubora ikiwemo shule na kwenda kupanga.

"Zipo sababu zinazochangia watumishi hawa kuhama katika nyumba hizo,ni tatizo la kishirikina na mizengwe katika nyumba hizo.

"Kwa hiyo hii ni sababu mojawapo hawapendi kuziacha na kwenda kupanga, ni vyema yakaachwa kusudi wapende kuishi kwenye nyumba hizo,"amesema Msongela.

Kwa mujibu wa madiwani hao, wameeleza katika baraza hilo kuwa, zipo baadhi ya nyumba kadhaa za walimu wilayani humo ambazo zimetelekezwa na kuachwa na watumishi hao ambao awali waliishi kwa muda mfupi na kwa sasa zimechakaa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news