Utalii wa Malikale washika kasi nchini, Wafaransa wafurika Kilwa kisiwani

NA BEATUS MAGANJA

KWA miongo kadhaa kumekuwa na dhana ya kwamba wageni wengi wa nje hupendelea zaidi utalii wa kuona wanyamapori, lakini hivi karibuni dhana hiyo imeanza kubadilika kwa kasi ambapo Tanzania imeanza kupokea wageni makundi kwa makundi wakitembelea katika maeneo yetu ya Malikale hususani Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara.
Ni takrikani siku tisa sasa katika kipindi cha mwezi Februari kuanzia tarehe 3 hadi 11, 2024, Tanzania kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeweza kushuhudia meli zilizosheheni makundi ya watalii kutoka mataifa mbalimbali zikipishana kutia nanga katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara na kufikisha idadi ya watalii wapatao 445 kwa safari nne za kitalii zilizofanyika.
Kwa mara nyingine Februari 11, 2024 TAWA ilipokea kundi la nne la watalii wapatao 114 kutoka Ufaransa ambao waliingia Kilwa kisiwani kwa ajili ya shughuli za utalii na kufanya idadi ya watalii wa nje waliotembelea hifadhi hiyo ndani ya siku tisa tu kuwa 445.

Hata hivyo, TAWA inategemea kuendelea kupata wageni wengi kutoka kona mbalimbali za Dunia kuja kutembelea na kutalii katika hifadhi hiyo kongwe yenye utajiri mkubwa wa kihistoria.
Kwa nini Kilwa kisiwani na Songo Mnara? Wahenga walisema ukitaka kuujua uhondo wa ngoma, uingie ucheze, hivyo TAWA inaendelea kuwakaribisha watalii wote wa ndani na nje kutembelea hifadhi hii kujionea yaliyomo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news