Uwanja wa Amaan Zanzibar waingia katika tuzo za mwaka Uwanja Bora Duniani

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameipa heshima ya kipekee Sekta ya Michezo nchini, kwani baada ya maboresho makubwa ya Uwanja wa Amaan jijini Zanzibar umeingia katika kiny'angany'ro cha viwanja vipya bora duniani.

Aleksander Hosny kutoka Uholanzi ambaye ni mwasisi wa tuzo za viwanja bora vya soka duniani kupitia StadiumDB.com amesema, uwanja huo ambao kwa sasa unatambulika kama New Amaan Sports Complex unastahili kutwaa tuzo ya uwanja bora kwa mwaka 2023.

Amesema,New Amaan Sports Complex umeingia katika orodha ya viwanja 35 bora duniani ambavyo vinawania tuzo hiyo ya ubora.Bonyeza hapa kupigia kura Amaan Stadium》》》

"Ninaamini kura za mashabiki zinaweza kuamua kuwa Uwanja wa Amaan ni namba moja duniani kati ya viwanja 35 vilivyoingia kwenye kiny'ang'anyiro kutoka kote duniani.

"Na Uwanja wa Amaan kutoka Zanzibar bila shaka ni miongoni mwa viwanja vya kuvutia vilivyokamilika mwaka 2023 katika sehemu hii ya Dunia."

Amesema, uwanja huo si fahari tu kwa wananchi wa Zanzibar bali hata nje ya Afrika na wapenda soka duniani.Bonyeza hapa kupigia kura Amaan Stadium》》》

"Kwa hiyo, Uwanja wa Amaan ndio pekee ulioingia katika kinyangany'ro kutoka Tanzania katika mashindano ya mwaka huu.

"Huenda kukawa na ushindani mkali kati ya mwakilishi wa Tanzania na Stade Nelson Mandela kutoka Baraki, Algeria."

Uwanja wa Mwaka ni nini? Mashindano ya Uwanja wa Mwaka duniani ni hutokana na kura ya umma ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka tangu 2011.Bonyeza hapa kupigia kura Amaan Stadium》》》

Aidha,tuzo hiyo ni matokeo ya kura nyingi zaidi za umma na aina yake duniani.

Tangu toleo la kwanza lianze, jumla ya kura halali zaidi ya 400,000 zimehesabiwa.

Awali Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi alisema, Serikali ya Zanzibar itaendelea kuweka mazingira bora ya michezo ili kuimarisha vipaji vya wanamichezo.Bonyeza hapa kupigia kura Amaan Stadium》》》

Alisema,azma ya Serikali ni kuimarisha sekta ya michezo kwa kuendeleza na kuibua vipaji vya wanamichezo ili kuleta maendeleo nchini.

"Sasa hivi hatuna shaka vipaji tunavyo vya michezo mbalimbali tunachohitaji mazingira bora,"alisema Dkt.Mwinyi.Bonyeza hapa kupigia kura Amaan Stadium》》》

Aidha, alieleza kuwa uwanja huo utatumika kwa michezo ya aina mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, judo, mpira wa kikapu, mpira wa wavu, mpira wa mkono, na mingineyo.

Dkt. Mwinyi aliipongeza Kampuni ya Orkun ya Uturuki kwa juhudi waliyoifanya ya kukamilisha ujenzi wa uwanja huo kwa wakati na kwa kiwango cha kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news