VIDEO:Wajumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini wabainisha mengi

"Tumekutana kwa mara ya kwanza na tumeweka malengo yetu kwamba ni lazima tushirikiane tuweze kufanikisha majukumu ambayo tumepewa. 

"Bado kuna maeneo mengi vijijini hayana umeme. Kwahiyo naamini hiyo ndiyo itakuwa kazi yetu kubwa kuhakikisha kwamba maeneo mengi ambayo hayajafikiwa yanafikiwa ili kuleta maendeleo vijijini. Siyo umeme tu bali pamoja na aina nyingine za nishati,"Mhandisi Sophia Mgonja,Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini-Feb.2024;
"Tunashukuru kwa kuaminiwa na Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ametukopesha imani, mimi pamoja na wenzangu tutamlipa kwa usimamizi mzuri wa taasisi. 

"Tukiongozwa na Mwenyekiti wetu tutaisimamia REA itekeleze majukumu yake kama ambavyo imekusudiwa katika Sheria ya REA ya Mwaka 2005,"Mhandisi Ahmed Chinemba,Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini-Feb. 2024;
"Ninaahidi nitatumikia nafasi hii kwa juhudi na weledi katika kulinda maslahi mapana ya Taifa letu,"Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Mwantum Issa Sultan-Feb.2024;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news