Wafanyakazi wa Afya ya Jamii (CHW) waanza kutambuliwa kwa vitendo

ZANZIBAR-Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Hassan Khamis Hafidh amesema,Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kuwatambua Wafanyakazi wa Afya ya Jamii (CHW) kwa vitendo.
Ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na stahiki za malipo kwa wafanyakazi hao, huko Ofisi za wizara hiyo Mnazimmoja Mjini Unguja.

Alieleza kuwa,taratibu zote za kazi na malipo kwa wafanyakazi hao zinaendelea kufanyiwa kazi na Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kinga baada ya kurasimishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt. Hussein Ali Mwinyi kutoka Wahudumu wa Afya wa Kujitolea (CHV) kuwa wafanyakazi wa Afya ya Jamii (CHW) Desemba 16,mwaka jana.

“Kuanzia mwezi Januari,2024 stahiki za wafanyakazi wetu hawa zitatoka, Wizara ya Afya kupitia idara yetu ya kinga,”alifafanua Naibu Waziri.

Aidha, alisema kwa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na wafanyakazi hao katika kutoa huduma za afya kwa jamii wizara imejipanga kuwaboresha wafanyakazi hao kwa kuwapatia mafunzo ya miezi sita yatakayoambatana na mitihani ili kuimarisha utendaji wao.

Zaidi ya wafanyakazi 2000 wamerasimishwa kutoka Wahudumu wa Afya ya Jamii wa Kujitolea (CHV) na kuwa wafanyakazi wa Afya katika Ngazi ya Jamii (CHW), ambapo awali walikua wakipata stahiki zao kupitia Taasisi ya D-tree.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news