Waganga wafawidhi kuanza kulipwa posho ya madaraka

DODOMA-Serikali kupitia Wizara ya Afya imesema, kuanzia mwaka wa fedha ujao waganga wafawidhi katika vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi wataanza kupewa posho ya madaraka kwa kazi kubwa wanayofanya.
Akizungumza katika Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wafawidhi wa Vituo vya kutolea huduma za afya ngazi ya msingi, Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema, waganga wafawidhi wanastahili kulipwa posho hiyo na ameahidi kuanzia Julai,2024 itaanza kutolewa kwa wataalam hao muhimu.
Amesema,Wanganga Wafawidhi wanafanya kazi kubwa kwenye vituo vya kutolea huduma.


"Ninyi ndio madaktari, wafamasia, wataalam wa maabara, mnasimamia ujenzi wa miradi ya serikali hakika mnastahili kulipwa posho hii naenda kuonana na wadau na katika fedha tutakazopata kiasi kitatumika kwa ajili ya kulipa posho hii.
"Na kwa kuwa sasa ndio tunaendelea na michakato ya bajeti posho hii iingizwe kwenye mipango yetu iwe rasmi na watalaam wetu hawa wapate posho hii," amesisitiza Mhe. Ummy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news