Watalii wazidi kumiminika Kilwa,TAWA yatoa neno

NA BEATUS MAGANJA

IDADI ya watalii wa kigeni kutoka Mataifa mbalimbali Duniani inazidi kuongezeka kwa Kasi katika Hifadhi ya Urithi wa Dunia ya Magofu ya Kilwa kisiwani na Songo Mnara, Hifadhi inayotajwa kuwa na upekee wa utalii wa kihistoria na kiutamaduni.
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA ikiwa ndiyo taasisi yenye dhamana ya usimamizi wa Hifadhi hiyo, leo Februari 15, 2024 imepokea kundi la 5 la Watalii 119 kutoka Mataifa mbalimbali Duniani ikiwa ni mfululizo wa safari za watalii wa nje kutembelea hifadhi hiyo kwa shughuli za utalii.

Watalii waliowasili leo wanatajwa kutoka katika nchi za Uingereza, Ufaransa Ujerumani, Italia, Ubelgiji, Hispania na Canada wakisafirishwa na meli iitwayo Le Bougainville huku Kampuni ya kitalii ya Akorn Destination Management (A&K) ikiwa ndiyo mratibu wa safari hiyo.
Haya ni matokeo ya hatua za makusudi zilizofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Sekta ya utalii nchini inakua kwa kasi baada ya kucheza filamu maarufu iitwayo Tanzania The Royal Tour.
Pia jitihada za dhati zilizofanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TAWA katika kuboresha miundombinu wezeshi ya utalii katika Hifadhi hiyo kama vile ujenzi wa ghati, sehemu za malazi, maeneo ya kupumzikia wageni, njia za kutembelea wageni kuelekea katika vivutio lakini pia ubora wa huduma kwa watalii unaotolewa na watumishi wa TAWA katika Hifadhi hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news