Watanzania tumeyapuuza yaliyotabiriwa na Mwinjilisti Temba?

DAR ES SALAAM-Mwinjilisti na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba tarehe 31 Desemba, 2023 alitoa unabii wa namna mwaka 2024 utakavyokuwa na ajali nyingi zikihusisha malori na magari madogo ambazo zitateketeza uhai wa watu wengi.

Huku akiwataka Watanzania kumlilia Mungu na kuhakikisha wanavunja roho za mauti nchini.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni kwa macho yetu tumeshuhudia Jiji la Arusha unabii huo ukitimia baada ya kutokea kwa ajali iliyohusisha Lori na magari madogo na kusababisha vifo vya watu 25 na majeruhi kadhaa ikijumuisha watu wa ndani na nje ya nchi.

Hivyo kufuatia ajali hiyo pia tumeona baadhi ya wanaharakati, watetezi wa haki za binadamu akiwemo Onesmo Ole Ngurumwa akipaza sauti yake na kwa mara ya kwanza licha ya kwamba idadi ya waliofariki na kujeruhiwa sio kubwa kuzidi ajali nyingine zilizopita,

Ila kwa sababu ya unabii huo kumejitokeza wanaharakati hao kutishia kuipeleka mahakamani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili Mahakama ielekeze kutungwa Sheria itakayozuia malori kupita barabarani nyakati za mchana hususani katikati ya majiji.

Hata hivyo, ni kwamba maneno hayo hayo yanayozungumzwa na wanaharakati hao hao yamekuwa yakizungumzwa kila kukicha na Muhubiri huyo ambaye Mungu amempa macho ya kuona mbali.

Kwani amekuwa akipiga kelele na kupaza sauti mara kwa mara mpaka baadhi ya watu wakaendelea kuliona kama jambo la kawaida pale alipoanza kunena na kusema malori yasiruhusiwe kuingia jijini Dar es Salaam kwa wingi,kwani yatakuja kuleta ajali mbaya.

Mwinjilisti Temba aliweka wazi kuwa malori hayo yanapaswa kuishia Chalinze na Vigwaza mkoani Pwani huku akishauri mengine yakashushe na kupakia mizigo yao katika Bandari Kavu ya Kwala, na jambo hilo alilihamasisha kwa kelele kubwa na kulalamika baada ya malori kuendelea kujaa jijini Dar es Salaam hususani katika Daraja la Ubungo.

Muhubiri huyo alinyanyuka kwa ujasiri mkubwa na kulikemea jambo hilo na kuiomba Serikali kuamuru malori yaende Kwala, na tangu aliponena hayo ni kwamba mizigo mingi ya Malori hususan ya kutoka nchini Burundi ni wiki ya tatu sasa imeanza kupelekwa kwenye Bandari Kavu hiyo, ambapo pia Malori hayo yamekuwa yakipakia mizigo hiyo kila kukicha kutoka Kwala.

Na baadhi ya waandishi wa habari waliotembelea Bandari Kavu ya Kwala walithibitisha jambo hilo, kwamba mizigo kwa sasa inatoka Kwala na Msemaji wa Serikali, Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) waliweza kuthibitisha suala hilo kwamba mizigo sasa imeanza kupelekwa na kupatikana Kwala.


Haya yote yanatokea kutokana na Juhudi binafsi za maono aliyonayo Mwinjilisti wa Kimataifa Alphonce Temba.

Hivyo baada ya ajali hiyo ya jijini Arusha kutokea, wapo Watanzania wengi hususan wanaofuatilia tovuti hii wameomba Serikali kwamba ni muda sasa iwatumie viongozi wa dini wenye karama kubwa kama Mwinjilisti Temba pasipo kuangalia dini zao ili kusaidia kulinusuru Taifa na majanga kama hayo.

Wanasema ingekuwa ni mataifa mengine Mtumishi kama Mwinjilisti Temba tayari Serikali ingekuwa imemuita na kukaa naye ili atoe mwelekeo wa namna gani jamii ipone na sio Serikali kuendelea kuamini kuwa wapo viongozi wa Dini huku inashindwa kuwatumia kwani ni jambo la kushangaza sana.

Wamedai ni jambo la kushangaza,kwani wapo wananchi jijini Arusha waliolalamika kwa nini Serikali haikumpeleka Mwinjilisti Temba jijini humo hata angalau kwenye mazishi ya waliofariki katika ajali hiyo ili kwa kuwepo kwake kuendelee kufanyika dua na maono kwa sababu yeye ndiye aliyefunuliwa.

Hata katika Bibilia inaelezwa kuwa Mussa ndiye aliyefunuliwa kwenda kumtetea ndugu yake ili asiuawe na Wafilisti na ndiyo huyo huyo ambaye Mungu alimtumia baada ya miaka 40 kwenda kuwatoa wana wa Israeli katika Utumwa.

Hivyo leo hii jambo hilo limeletwa, kuna watumishi wengi wanatabiri mambo mengi, lakini kwenye hili Mwinjilisti wa Kimataifa hakuna asiyeamini kwamba alionyeshwa na Mungu na akaelezea nini cha kufanyika hususan maombi kwa dini zote.

Serikali yafaa kumtafuta na kumuunga mkono Mwinjilisti Temba ili atembee nchi nzima ayaongoze maombi hayo kwa wale wa jamii yake na jamii nyingine zikiendelea kujiongoza kutokana na imani zao ilmaradi tu Mungu alinena kupitia kinywa cha Mtumishi wa Mungu huyo.
Kama ilivyokuwa katika Awamu ya Tatu ya Serikali ya Hayati Benjamin Mkapa ambapo mwaka 1997, Serikali ilimsaidi Nabii Kenneth Mwasumbi aliyezunguka nchi nzima tena kipindi cha mvua za Elinino baada ya kutabiri na kuanzisha maombi ya Tanzania itubu yaliyohitimishwa katika mkutano mkubwa uliofanyika kwenye viwanja vya Mnazimmoja Dar es Salaam.

Mtumishi huyo tumeona akifanya kazi hizi za kiroho katika mataifa mbalimbali kama Zambia, Botswana, Nigeria, Ghana, Kenya na nchi nyingine nyingi.Soma utabiri wote hapa》》》

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news