Watendaji wa Kampuni ya PREZZIDAR washitakiwa kwa uhujumu uchumi Kinondoni

DAR ES SALAAM-Watendaji wa kampuni ijulikanayo kwa jina la PREZZIDAR iliyokuwa inajihusisha an ukusayaji ushuru wa masoko katika Halmashauri ya Manispaa ya Kindononi
Mkoa wa Dar es Salaam wameshtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kwa tuhuma za uhujumu uchumi,ubadhirifu pamoja na kusaidia kutenda kosa la kuongoza genge la uhalifu.

Mbali na makosa hayo,watendaji hao pia wameshtakiwa kwa kosa la uchepushaji wa mapato ya ushuru na kufunguliwa kesi namba 1648/2024.

"Ofisi pia imefanya uchunguzi kuhusiana na mapato na kubaini kuwa watendaji wa kampuni hiyo ya PREZZIDAR wamekuwa wakihujumu mapato kwa kutotumia POS mashine ipasavyo, hivyo basi tarehe 10 mwezi wa kwanza mwaka huu watendaji wameshtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kinondoni, Ismail Selemani amesema kuwa, taasisi hiyo kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni pamoja na ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo walifanya ufuatiliaji na kubaini kampuni iliyopewa jukumu la kukusanya ushuru wa masoko ya Manispaa imekuwa ikifanya udanganyifu katika ukusanyaji na uwasilishaji wa mapato hayo benki.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya utendaji ya kipindi cha miezi mitatu kutoka Oktoba 2023 mpaka Desemba 2023.

Vile vile ametoa wito kwa wafanyabiashara kuzingatia miongozo inayotolewa na halmashauri na Serikali kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kulipa ushuru na kuhakikisha wanapatiwa stakabadhi sawa na walichotoa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news