Waziri Mkuu aweka jiwe la msingi ujenzi jengo la WMA
DODOMA-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA).
Ujenzi wa jengo hilo utagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 6.17 na linatarajiwa kukamilika ifikapo Januari,2025.