DODOMA-Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula la Duniani (World Food Programme -WFP) limesema litaendeleza ushirikiano na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuhakikisha masuala ya menejimenti ya maafa yanaendelea kutekelezwa kwa tija na malengo yaliyokusudiwa.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao chache na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula la Duniani (World food Programme -WFP), Bw. Brian John Bogart alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa nchini.
Ni kwa kuimarisha uwezo wa kitaalamu na Kiteknolojia kwa kutumia teknolojia za kisasa.
Hayo yameelezwa na Naibu Mkurugenzi wa shirika hilo, Bw. Brian John Bogart alipokutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu, Dkt. Jim Yonazi ofisi kwake jijini Dodoma.
Amesema kuwa, wataendelea kutoa ushirikiano hususani katika kuwajengea uwezo juu ya matumizi vifaa vya kiteknolojia ya kisasa ya kuchukua matukio na tarifa mbalimbali kwa kutumia vifaa aina ya ndege nyuki (drones) pamoja na kufadhili vifaa hivyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi akisalimiana na Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula la Duniani (World food Programme -WFP), Bw. Brian John Bogart alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa nchini.
Aidha, wataendelea kutoa mafunzo kuhusu masuala ya uchambuzi wa taarifa (Data Analysis) ili kuwa na utaalamu wa kutosha katika kuchambua taarifa zinazokusanywa kupitia vifaa hivyo (drones) kwa ajili ya kuboresha na kuwa na ufanisi zaidi kwa kutumia teknolojia hiyo ya kisasa.
"Tumeendelea kutoa elimu na tutafanya mafunzo kwa wataalam wetu ili kuwa na ujuzi katika kuchambua taarifa pamoja na matumizi ya drone na kuzitafsiri taarifa kama inavyotakiwa,"ameeleza.
Naye Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dkt. Jim Yonazi amewashukuru WFP huku akisema ofisi yake itaendelea kutoa ushirikiano hasa katika kipindi hiki cha mvua nyingi zenye kuleta maafa nchini kwa kuzingatia umuhimu wa taarifa na matukio hayo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi wa WFP (World Food Programme), Bw. Brian John Bogart (wa tatu kutoka kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Brigedia Jenerali Hosea Ndagala (wa kwanza kulia) pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara hiyo Luteni Kanali Selestine Masalamado (wa kwanza kushoto) alipomtembelea ofisini kwake na kufanya mazungumzo kuhusu masuala ya menejimenti ya maafa nchini.(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).
"WFP mmeendelea kuwa mstari wa mbele kuungana na Serikali hususani katika masuala ya Menejimenti ya Maafa, niendelee kutoa wito kwa wadau wengine pia kuunga mkono jitihada za Serikali katika masula mbalimbali nchini," amesema Dkt. Yonazi.
Tags
Habari
Mpango wa Kukabili Maafa
Ofisi ya Waziri Mkuu
WFP
WFP Tanzania
World Food Programme (WFP)