ACCRA-Mashindano ya Afrika (All African Games 2023) yamezinduliwa rasmi Machi 8, 2024 Jijini Accra, Ghana yakiongozwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Nana Akufo Addo, huku yakishuhudiwa na Wanamichezo kutoka Mataifa 54 ikiwemo Tanzania na kupambwa na maandamano pamoja na burudani mbalimbali.

