NA ABEL PAUL
Tanpol
ASKARI Polisi wa kike Kikosi cha Mbwa na farasi makao makuu Dar es salaam wameendelea kuyakumbuka makundi ya wahitaji licha ya kuwa na dhamana ya kuwalinda raia na mali zao ambapo wamewafariji wagonjwa katika Hospitali ya Zakhiem iliyopo Mbagala Wilaya Temeke Mkoa wa Dar es salaam na kutoa vitu mbalimbali.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Khadija Maulid ambaye aliwaongoza askari wa kike kwenda hospitali ya zakhem kutoa misaada ya vitu mbalimbali ambavyo waliona vitakuwa msaada kwa wahitaji hao ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
Ameongeza kuwa, kuelekea Siku ya Wanawake Duniani wameona ni vyema wao kama kundi la askari wa kike wa kikosi cha Mbwa na farasi kuliangalia kundi hilo la wahitaji na kutoa kile walichobarikiwa kutoa kwa wahitaji hao.
Mkaguzi huyo amebainisha kuwa wamekuwa na utaratibu huo mara kwa mara kama kikosi Cha Mbwa na farasi Makao Makuu ambapo wamekuwa wakitembelea makundi mbalimbali ya wahitaji katika jamii.
Pia,Mkaguzi Khadija ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi kufika Makao Makuu ya kikosi cha Mbwa na farasi kujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na wanyama Mbwa ambao wamekuwa wakiwatumia katika ulinzi wa makazi yao.