ATCL yafikisha ndege 13 huku nyingine zikiwa njiani

NA GODFREY NNKO

SERIKALI imeendelea kuliimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kuwekeza zaidi ikiwemo kununua ndege ili kulifanya limudu kutoa huduma na kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za kiuchumi.
Msemaji Mkuu wa Serikali,Mobhare Matinyi ameyasema hayo leo Machi 24,2024 jijijni Dar es Salaam wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarani.

Amesema,katika miaka mitatu Serikali imenunua ndege tano zikiwemo tatu za masafa ya kati ambazo ni Airbus A220 mbili, Boeing 737 Max9, Boeing 767-300F ya mizigo na Dash 8 Q-400 na zote zinaendelea kutoa huduma.

“Ndege mbili zaidi Boeing 737 Max9 (iko katika hatua ya makabidhiano) na moja ya masafa marefu aina ya Boeing 787-8 (katika hatua ya uundwaji) tayari zimeshanunuliwa na zinatarajiwa kuwasili nchini mwezi Machi na Aprili mwaka huu.

“Hivyo basi, kwa kujumuisha na uwekezaji huu sasa ATCL ina jumla ya ndege za abiria 12 na moja ya mizigo zinazohuduma vituo 24 kutoka vituo 19 vya mwaka 2021 na inatarajiwa vitaongezeka.

“Kwa ujumla wake, ATCL imeongeza abiria kutoka 537,155 mwaka 2021 hadi 1,070,734.

"Tani za mizigo 1,290 mwaka 2021 hadi 3,561; na miruko 10,550 mwaka 2021 hadi 17,198 mwaka 2023,” amesema Matinyi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news