MAPUTO-Mheshimiwa Phaustine M. Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Maputo alikutana na Balozi wa Jamhuri ya Kongo (Congo Brazzaville), Mhe. Constant-Serge Bounda tarehe 11 Machi, 2024 kwenye Ofisi za Ubalozi zilizopo Jijini Maputo.

Wakati wa mkutano huo, Viongozi hao wawili walizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili pamoja na masuala mengine yanayohusu Ushirikiano wa Kikanda.