Balozi Mussa aongoza Ujumbe wa Tanzania katika kikao cha Kamati ya Fedha SADC


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa ameendelea kuongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kikao cha Kamati ya Fedha ya Jumuiya ya Maendeleo Kusaini mwa Afrika (SADC) kinachofanyika Jijini Luanda, Angola tarehe 6 Machi, 2024.

Pamoja na masuala mengine, kikao hicho kimepokea na kujadili taarifa ya Kamati Ndogo ya Fedha ya SADC na Kamati ya Ukaguzi ambapo ajenda mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo mpango wa bajeti ya kanda kwa kipindi cha 2024/2025 na mapendekezo yake yatawasilishwa katika Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kuidhinishwa tarehe 10 na 11 Machi, 2024.
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Fedha za Nje kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw, Rished Bade, Afisa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Joseph Haule na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Noah Mboma wakifuatilia majadiliano katika Kikao cha Kamati ya Fedha cha SADC kinachoendelea jijini Luanda, Angola tarehe 6 Machi, 2024.
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikifuatilia majadiliano ya Kikao cha Kamati ya Fedha kinachoendelea jijini Luanda, Angola tarehe 6 Machi, 2024.
Balozi Mussa akiteta jambo na sehemu ya wajumbe wa kikao hicho kutoka Tanzania na Afrika Kusini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news