DODOMA-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ikiongozwa na Gavana Emmanuel Tutuba, imefuturisha wakazi wa jiji la Dodoma ambapo wageni mbalimbali wamehudhuria hafla hiyo wakiwemo viongozi wa serikali na dini, taasisi za fedha, makundi maalumu, vituo vya watoto yatima pamoja na wafanyakazi wa Benki Kuu.
Gavana Emmanuel Tutuba akipewa maelezo na mhudumu kuhusu aina za uji uliopo katika hafla ya futari iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 26 Machi 2024 katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo, Gavana Tutuba amewasihi viongozi wa dini na wananchi wote kuliombea taifa liendelea kuwa na utulivu, mshikamano na amani ili kuwawezesha wananchi kuendelea kufanya kazi kwa ustawi na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Wageni waalikwa wakipata futari katika hafla iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.
Gavana Emmanuel Tutuba akifurahia jambo alipowasili katika hafla iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Naibu Gavana, Bi. Sauda Kassim Msemo, Meneja Idara ya Mawasiliano, Bi. Victoria Msina, Mkurugenzi wa Tawi la BoT Dodoma, Dkt. Wilfred Mbowe, na Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano, Bi. Noves Moses.
Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.
Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Gavana Emmanuel Tutuba wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.
“Baraka tunazoendelea kuzipokea kama nchi inawezekana zinatokana na maombi ya kila mmoja wetu,” alisema.
Gavana Emmanuel Tutuba katika picha ya pamoja na watoto kutoka vituo vya watoto yatima vya jijini Dodoma.
Gavana Tutuba aliongeza kuwa katika ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania imekua na uchumi imara zaidi pamoja na uwepo wa changamoto mbalimbali za kiuchumi duniani.
Naibu Gavana (Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha), Bi. Sauda Kassim Msemo, akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.
Kwa upande wake Naibu Gavana (Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha), Bi. Sauda Kassim Msemo, alisema kuwa Benki Kuu kama ilivyo kwa taasisi nyingine nchini, huandaa hafla kama hii ya leo, kwa wafanyakazi wake, lakini pia kwa kuwaalika wadau wake mbalimbali ili kujumuika kwa pamoja na kumshukuru Mwenyezi Mungu.
Mchungaji John Kamoyo kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajab Shabani, akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.
Wakizungumza awali, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajab Shabani na Mchungaji John Kamoyo kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) wameipongeza Benki Kuu kwa kuandaa hafla hiyo iliyohusisha makundi mbalimbali katika jamii na kusisitiza umuhimu wa waumini wa dini zote kuendelea kushirikiana katika kujenga na kukuza uchumi wa nchi yetu.