Bodi ya Bima ya Amana yatoa taarifa njema kwa waliokuwa wateja wa Meru Community Bank

ARUSHA-Bodi ya Bima ya Amana imetangaza kwamba wale wote waliokuwa wateja katika Benki ya Wananchi Meru (Meru Community Bank) ambao hawajachukua amana zao zilizokuwa chini ya Shilingi 1,500,000 wafike katika tawi la Benki ya Biashara Tanzania (TCB) tawi la Meru au Tawi la Benki Kuu Arusha kwa ajili ya kurudishiwa amana zao.
Wakufunzi wa DIB wakiwa wamejipanga kwa ajili ya kutoa elimu kwa Wakulima wa Kijiji cha King’ori.

Hayo yamesemwa na Meneja Uendeshaji wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Nkanwa Magina wakati wa mfululizo wa mafunzo kuhusiana na uwepo wa DIB.

Majukumu ya DIB na mfumo wa DIB, mafunzo yakielekezwa kwa makundi mbalimbali wilayani Meru hususani kwa viongozi wa vijiji, na wafanyakazi wa taasisi mbalimbali za serikali.Meneja Uendeshaji wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Nkanwa Magina akiwasilisha mada.

Pia makundi mengine ni pamoja na wafanyabiashara kwenye minada na masoko mbalimbali ya wazi ambayo yapo katika vitongoji vya King’ori, Kikatiti, Maji ya Chai, Usa River na Leganga.
Wafanyakazi wa Halmashauri na Viongozi wa vijiji wakifuatilia mada.

Aidha, mafunzo hayo yaliendeshwa kwa takribani wiki nzima na kufikia tamati leo.
DIB walitoa elimu kwa umma kwa kupitia redio maarufu ya Safina FM Arusha, pichani Meneja Uendeshaji, Nkanwa Magina (kushoto) na Mhasibu Mwandamizi, Silvani Makole wakitoa mada.

Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru, Dkt. Amani Sanga, aliishuku DIB kwa kuleta elimu hiyo katika muda muafaka.
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru, Dkt. Amani Sanga akifungua mafunzo ya DIB kwa wafanyakazi na viongozi wa vijiji mbalimbali vya Halmashauri ya Meru.

“Wananchi wengi waliopo katika Wilaya ya Meru walikuwa wamekata tamaa ya kuhifadhi fedha zao katika taasisi za fedha baada ya kuanguka kwa benki waliyokuwa wanaitumainia na kuipenda ya Meru Community Bank. 

"Mimi nikiwa mmoja wa wahanga waliopoteza fedha zao baada ya kufungwa kwa benki yetu ya Meru, najisikia fahari leo hii kusikia kwamba hatimaye sasa ninaweza kwenda kupewa amana yangu katika tawi la benki ya TCB,” amesema.Mhasibu Mwandamizi wa DIB, Silvani Makole akiwasilisha mada kuhusu Ufilisi wa Benki ya Wananchi Meru mbele ya wafanyakazi pamoja na viongozi wa vijiji wa Wilaya ya Arumeru.

Aliwaasa wananchi wote kuziamini taasisi za fedha ambazo zina leseni ya Benki Kuu ya Tanzania kwa sababu amana zao zinalindwa na Bodi ya Bima ya Amana.
Mwenyekiti wa Kamati ya kuongoza waliokuwa na amana katika Benki ya Wananchi Meru, Godwin Nderingo, akitoa neno la shukuran baada ya mafunzo.

Naye kiongozi wa Kamati Teule ya Kusimamia Ufilisi upande wa Waliokuwa Wateja wa Benki ya Wananchi Meru, Godwin Nderingo aliipongeza DIB kwa kufanya kazi yao kwa waledi mkubwa ili kuwahakikishia wananchi wanapata haki zao.
Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi wa DIB, Joyce Shala akimuelimisha mfanyabiashara na mteja wa zamani wa benki ya Meru katika soko la Leganga - Usa River.

“Ingawa muda umekuwa mrefu sasa yapata miaka sita tokea kufungwa kwa benki hii na zoezi la ufilisi likiwa limefikia asilimia 70, ni ushauri wetu sisi tuliokuwa wateja kuwaomba watu wote waliokuwa wanadaiwa na benki hii kurudisha fedha walizokopa ili zoezi hili lifikie mwisho.”
Elimu sokoni Tengeru ikiendelea.

Wakati wote wa mafuzno wananchi walifurahia zawadi mbalimbali zilizokuwa zikitolewa ikiwa ni pamoja na majibu ya maswali yao yaliyokuwa yakijibiwa kwa umahiri na wakufunzi wasaidizi, Joyce Shala na Sylvani Makole.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news